JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE
Kumb. Na. HWC/A.11/22/68
Tarehe: 02/06/2025
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa ya kujaza nafasi zilizotolewa na kibali chenye Kumb.Na FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (Office Management Secretary II) – NAFASI 05
1.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuchapa barua, taarifa, nyaraka za kawaida na za siri.
ii. Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.1.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) ya Uhazili na awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Programu ya Kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali ya TGS C kwa mwezi.
1.2 DEREVA DARAJA LA II (Driver II) – NAFASI 04
1.2.1 KAZI NA MAJUKUMU
i. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za udereva.
ii. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali kwa kuzingatia maelekezo utakayopewa na msimamizi wako wa kazi.
iii. Kutunza na kuandika daftari la safari (log-book) kwa safari zote.
iv. Kufanya matengenezo ya madogo madogo ya magari.
v. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote.
vi. Kutekeleza kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI), awe na leseni Daraja C au E ya uendeshaji wa magari, ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja, awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na VETA au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali ya TGS B kwa mwezi.
MASHARTI KWA JUMLA
i. Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
iv. “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (Form IV na VI result slip) HAZITAKUBALIWA.
v. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
vi. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Postgraduate/degree/advanced diploma/diploma/Certificates, Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI, Computer certificate, Vyeti vya taaluma (Professional Certificate from respective Board).
ix. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
x. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15/06/2025.
xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI (W),
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE,
S.L.P 65, CHALINZE.
xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo:
👉 https://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xv. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Tangazo hili limetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE